Gavana Nyoro amteuwa naibu wake
Gavana wa Kiambu James Nyoro hatimaye amemteuwa Naibu Gavana na kujaza pengo ambalo limekuwapo tangu alipoingia ofisini kuwa kiongozi wa kaunti hiyo. Joyce Wanjiku, mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Gatundu Kusini, Joseph Ngugi, alitajwa Jumatano, Februari 19 kuchukua nafasi hiyo na sasa anasubiri kukaguliwa na kuidhinishwa na bunge la kaunti hiyo.